Home Habari za michezo KOCHA ALIYEIFUNGA SIMBA GOLI 4-0, AOMBA KIBARUA CHA UKOCHA MKUU MSIMBAZI…AHMED ALLY...

KOCHA ALIYEIFUNGA SIMBA GOLI 4-0, AOMBA KIBARUA CHA UKOCHA MKUU MSIMBAZI…AHMED ALLY ATOA VIGEZO…


Imeelezwa kuwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Gavin Hunt yupo kwenye rada za mabosi wa Simba ili achukue mikoba ya Pablo Franco.

Kocha huyo alikuwa kwenye benchi la ufundi Mei 15,2020 wakati timu yake ikishinda mchezo wa kwanza mbele ya Simba kwa mabao 4-0.

Kwa sasa kikosi cha Simba kipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola ambaye ni mzawa alikuwa na benchi hilo tangu zama za Sven Vandenbroeck.

Habari zimeeleza kuwa Simba inahitaji kocha mwenye uzoefu kwenye mechi za kimataifa ili iweze kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho na kufanya vizuri Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ahmed Ally Mkuu wa Kitengo cha Habari ndani ya Simba amesema kuwa wanahitaji kumpata kocha mpya ambaye atakuwa na ubora.

SOMA NA HII  KUFA KUFAANA KUTOKA KMC MPAKA SIMBA