Home Habari za michezo BAADA YA KUKABIDHIWA TIMU…MATOLA AANZA NA GIA KUBWA SIMBA…MUGALU NA LWANGA WAKIONA...

BAADA YA KUKABIDHIWA TIMU…MATOLA AANZA NA GIA KUBWA SIMBA…MUGALU NA LWANGA WAKIONA CHA MOTO….


Selenani Matola, Kocha Msaidizi wa Simba ambaye kwa sasa ni Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo ameanza kazi kwa kuwapa mbinu wachezaji wa timu hiyo kwa ajili ya mechi zilizobaki.

Ikiwa imecheza mechi 25 na kukusanya pointi 51 imebakiwa na mechi tano kukamilisha mzunguko wa pili na kufunga hesabu kwa msimu wa 2021/22.

Matola Juni 7 aliweza kuwaongoza mastaa wa timu hiyo ikiwa ni pamoja na mshambuliaji Chris Mugalu, kiungo Sadio Kanoute pamoja na Taddeo Lwanga kwenye mazoezi yaliyofanyika Viwanja vya Bunju.

Kwa wakati huu Simba ipo kwenye mchakato wa kumsaka kocha mpya ambaye atarithi mikoba ya Pablo kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23.

Mchezo ujao kwa Simba wa ligi ni dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Juni 16,2022.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Paul Nonga.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa malengo yaliyopo kwa sasa ni kumaliza ligi kwa kupata matokeo kwenye mechi zilizobaki.

SOMA NA HII  BAADA YA OKRAH...ANAYEFUATIA KUTAMBULISHWA YANGA NI HUYU HAPA...JAMAA ANAJUA MNOO..