Home Habari za michezo KIUNGO SIMBA AZURURA NA MKATABA MITAANI…MWENYEWE AWEKA MASHARTI YA KUUSAINI….

KIUNGO SIMBA AZURURA NA MKATABA MITAANI…MWENYEWE AWEKA MASHARTI YA KUUSAINI….


WAKATI Ligi Kuu Bara ikikaribia ukingoni, huku dirisha la usajili likianza kufunguliwa kinyemela kwa ajili ya msimu ujao, kiungo wa zamani wa Simba anayekipiga kwa sasa Ruvu Shooting, Abdulsamad Kassim anatembea na mkataba wake mfukoni.

Nyota huyo alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea Kagera Sugar na kulazimika kuvunja mkataba katikati ya msimu kutokana na kutopata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi hicho na kutimkia Ruvu na amekuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo katika duru hii ya pili.

Hata hivyo, kiungo kutoka Zanzibar, sasa anatembea na mkataba mpya wa maafande hao akisikilizia kusaini, kwani wakati anatua Ruvu alisaini miezi sita unnaomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa ameridhishwa na kiwango chake na kuwataka vigogo wa timuhiyo kumwongezea mkataba haraka kabla timu nyingine hazijaanza kuongea naye.

Hata hivyo inafahamika baada tu ya kauli hiyo ya Mkwasa, mabosi wa Ruvu walimfuata Abdulsamad na kumhakikishia mkataba mpya wa mwaka mmoja na kumtaka wakati wowote kwenda kusaini kama ataridhika nao lakini kiungo huyo hadi leo bado hajasaini.

Akizungumza  jana, Abdulsamad alieleza licha ya kupewa ofa hiyo na maafande hao wa Pwani lakini bado hajaamua kusaini kutokana na kusubiri msimu uishe ndio aamue.

Naye kocha Mkwasa alimuelezea kiungo huyo kwa kusema;”Ni kiungo mzuri, mwenye uwezo mkubwa na uzoefu wa kutosha bado namuhitaji kikosini kwa ajili ya misimu mingine ijayo.”

SOMA NA HII  YANGA SC YASHEREKEA UBINGWA..."SIMBA WATAKIMBIA UWANJANI...WALITUFUNGA MIDOMO