Home Habari za michezo PAMOJA NA KUPATA TIMU….NCHIMBI AFUNGUKA YALIYOMKUTA BAADA YA KUSEPA YANGA…

PAMOJA NA KUPATA TIMU….NCHIMBI AFUNGUKA YALIYOMKUTA BAADA YA KUSEPA YANGA…

Mshambuliaji mpya wa Fountain Gate ya Dodoma, Ditram Nchimbi amefunguka makukwa ailiyoyapitia ikiwa ni miezi kadhaa toka atoke Yanga.

Nchimbi amesema kuwa baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga alisajiliwa na Geita Gold kwa mwaka mmoja lakini mchezaji huyo hakuonekana sana huku kukiwa na taarifa mbalimbali.

Mshambuliaji huyo anaweka wazi alipata msiba lakini wakati huo huo alikuwa na maumivu ya ugoko kwa hiyo alipomaliza msiba alienda kufanya vipimo vya picha (xray) na kutakiwa kupumzika kwa wiki tatu hadi nne.

“Nikatuma taarifa kwa uongozi lakini mwisho wa siku ikachukuliwa tofauti, muda wa kurudi kazini ulipofika kuomba nauli sikutumiwa na wala simu zangu hazikupokelewa,” amesema Nchimbi na kuongeza;

“Mwisho walifunga mshahara wangu nikaona acha nikae kimya sikutaka iwe shida acha nipumzike na mkataba ukiisha nitaanza moja, nashukuru Mungu nikapona nikawa sawa kabisa.

SOMA NA HII  SIMBA WAMEPANIA AISEEE...WAPANGA KUMBEBA JUMLA JUMLA KIUNGO WA AL AHLY YA MISRI...