Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA NABI KUFUKUZWA YANGA….ALLY KAMWE AANIKA ‘CODE’ ZA UKWELI WA...

KUHUSU ISHU YA NABI KUFUKUZWA YANGA….ALLY KAMWE AANIKA ‘CODE’ ZA UKWELI WA MAMBO…

Habari za Yanga SC

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe ametolea ufafanuzi taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na kufukuzwa kwa kocha wao mkuu Nasreddine Nabi kutokana na kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.

Ally Kamwe amesema kwamba taarifa zinazosambaa ni mawazo na mitazamo ya wachambuzi wa soka hapa nchini na siyo msimamo wala mawazo ya uongozi wa klabu hiyo na hivyo basi wao wanamtambua Nabi kama kocha wao na hawana mpango wa kumfukuza kocha huyo.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUJIUNGA NA GEITA GOLD...JINA LA SAIDO NTIBAZONKIZA LATAJWA TENA YANGA...KAZE ASHINDWA KUJIZUIA...