Home Habari za michezo BAADA YA MBAMBAMBA NYIINGIII…HATIMAYE YANGA KUITUMIA SIMBA KUTINGA MAKUNDI CAF..

BAADA YA MBAMBAMBA NYIINGIII…HATIMAYE YANGA KUITUMIA SIMBA KUTINGA MAKUNDI CAF..

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amezungumza kuhusu maandalizi yao kuelekea mchezo wao wa mtoano ili kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Club Africain ya Tunisia ambao utachezwa Novemba 2, 2022 kwenye Dimba la Mkapa jijini Dar es salaam.

Kamwe amesema kwamba, maandalizi yao kuelekea mchezo huo yanaanza na mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Simba ambayo itachezwa siku ya Jumapili, Oktoba 23, 2022, na hivyo mechi hiyo itawapa kipimo sahihi cha maandalizi yao kuelekea mchezo huo wa Kimataifa.

Aidha, Kamwe anasema kwamba katika mchezo huo watatumia kila aina ya mbinu ambazo wamezipanga ili kuona kama zitaleta matunda katika mchezo huo na endapo kama zitaleta matunda, basi ndivyo jinsi watavyoondoka nazo kwenda kumkanda Mwarabu Novemba 2.

SOMA NA HII  : FURSA YA UTAJIRI NI SHINDANO LA EXPANSE KASINO NDANI YA MERIDIANBET....