Home Uncategorized MBWANA SAMATTA KUTUA BONGO HIVI KARIBUNI

MBWANA SAMATTA KUTUA BONGO HIVI KARIBUNI


MSHAMBULIAJI wa Aston Villa ya nchini Uingereza, Mtanzania Mbwana Samatta anatarajia kutua nchini wiki hii baada ya ligi ya nchini humo kufikia tamati mwishoni mwa wiki iliyopita.
Samatta ambaye timu yake ya Aston Villa imenusurika kushuka daraja msimu huu, imemaliza katika nafasi ya 17 ya msimamo wa Premier League ikiwa imeshinda michezo tisa huku ikitoa sare michezo saba na kupoteza michezo 21, hivyo imejikuta ikimaliza ikiwa na pointi 34.

Baba mzazi wa Samatta, Ally Samatta amesema kuwa, Samatta anatarajia kutua nchini ndani ya siku mbili hizi.Aidha Mzee Samatta alieleza kuwa, amefurahishwa kuona mtoto wake na timu yao ya Aston Villa kwa kuwa wamebaki kwenye Ligi Kuu England.

“Samatta anatarajia kurudi Tanzania kati ya kesho ama keshokutwa nadhani tutawasiliana ili nijue siku kamili atakayorejea, atakuja ndani ya siku mbili hizi kwa ajili ya kuiwahi mechi yake na Ali Kiba kwenye tamasha la SamaKiba watakayocheza Agosti 8.
“Amefurahi kuona amebaki ligi kuu, kwa upande wangu kama mzazi nimefurahi kuona mtoto wangu amefanikiwa kubaki Ligi Kuu ya England kwani nilikuwa nikiomba usiku na mchana,” alisema Mzee Samatta.

Chanzo:Championi
SOMA NA HII  YANGA YAPEPERUSHA POINTI SITA KATI 18 ILIZOKUWA IKISAKA, SARE TATU MFULULIZO