Home Uncategorized EYMAEL KUWATUMIA WACHEZAJI HAWA WATATU KUIMALIZA MBEYA CITY

EYMAEL KUWATUMIA WACHEZAJI HAWA WATATU KUIMALIZA MBEYA CITY

LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ataanza kuwatumia wachezaji wake wengine kesho mbele ya Mbeya City mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa saa 1:00 usiku.

Eymael amesema kuwa alikua na mpango wa kuwapa nafasi nyota wake watatu ambao ni Mrisho Ngassa, Tariq Seif na Kelvin Yondan kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting alibadili maamuzi kutokana na matokeo ambayo aliyapata.

“Ninatambua kwamba nina wachezaji wengi wazuri ila walishindwa kupata nafasi kwenye mchezo wetu dhidi ya Ruvu kutokana na kasi ya mpira ilvyokuwa na niliwapa majukumu mengine ya kuusoma mchezo.

“Bado tuna mechi nyingi nao wana umuhimu wataanza kuonyesha uwezo wao kwenye mechi zetu kikubwa ni sapoti ya mashabiki na kujua ni kipi ambacho wanatakiwa kukifanya uwanjani,” amesema.

SOMA NA HII  VIDEO: KOCHA KAZE AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOANZA MBELE YA SIMBA