Home Simba SC MABAO YA NAHODHA WA SIMBA JOHN BOCCO MBELE YA KAIZER CHIEFS YAMPA...

MABAO YA NAHODHA WA SIMBA JOHN BOCCO MBELE YA KAIZER CHIEFS YAMPA MILIONI


 LICHA ya kikosi cha Simba ambao walikuwa wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika kuishia hatua ya robo fainali, nahodha wa timu hiyo amepewa zawadi ya shilingi milioni mbili na nusu.

Bocco atapewa zawadi hiyo baada ya kuchaguliwa kuwa   Mchezaji Bora katika mchezo huo uliokuwa unakwenda kwa sera ya ‘Ama Zetu Ama Zao’ na ngoma ilikamilika Simba 3-0 Kaizer Chiefs.

Nahodha huyo mzawa atapewa zawadi hiyo ya milioni mbili na nusu (Sh 2,500,000) kutoka Kampuni ya Emirate Aluminium kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Simba kupitia ukurasa wa Instagram.

Bocco jana Mei 22 alikuwa kwenye ubora wake ambapo aliweza kufunga jumla ya mabao mawili dakika ya 23 na 55 huku bao la tatu likifungwa na Clatous Chama dakika ya 86.
Ushindi huo unaifanya Simba kuaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu ilikuwa ni hatua ya mtoano na anayeshinda ni yule mwenye idadi kubwa ya mabao.

Hivyo agregate kwa sasa katika hatua ya makundi inasoma Simba 3-4 Kaizer Chiefs kwa sababu mchezo wa awali, Mei 15, Uwanja wa FNB, Simba ilipoteza kwa kufungwa jumla ya mabao 4-0. 
SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO...BOCCO AZINDUKA ...AHMED ALLY AFUNGUKA JINSI ATAKAVYOTUMIWA....