Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO…BOCCO AZINDUKA …AHMED ALLY AFUNGUKA JINSI ATAKAVYOTUMIWA….

KUELEKEA MECHI YA KESHO…BOCCO AZINDUKA …AHMED ALLY AFUNGUKA JINSI ATAKAVYOTUMIWA….


MSHAMBULIAJI na Nahodha wa Simba, John Bocco, anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuelekea Kariakoo Dabi.

Dabi hiyo inatarajiwa kuzikutanisha timu kongwe hapa nchini za Yanga na Simba, mchezo utakaopigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Bocco aliikosa michezo kadhaa iliyopita ya Simba ikiwemo ya kimataifa kutokana na kuuguza majeraha ya goti.

 Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema Bocco ameingia kambini Jumatano kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga.

Ally alisema mshambuliaji huyo alifanya mazoezi ya pamoja na wenzake kujiandaa na mchezo huo, huku akibainisha kwamba, kwa sasa kikosi chao kina majeruhi mmoja ambaye ni Hassani Dilunga.

“Kikosi chetu kimeingia kambini leo (juzi) tayari kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa dabi dhidi ya Yanga tutakaocheza Jumamosi hii.

“Wachezaji wote wameingia kambini isipokuwa Dilunga ambaye alienda Sauzi kupatiwa matibabu ya goti.

“Bocco ni kati ya wachezaji walioingia kambini kujiandaa na mchezo huo baada ya kupona majeraha yake ya goti yaliyomuweka nje ya uwanja muda mrefu,” alisema Ally.

SOMA NA HII  BREAKING: SHOMARI KAPOMBE ASAINI MKATABA MPYA SIMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here