Home Habari za michezo BAADA YA OKRAH…ANAYEFUATIA KUTAMBULISHWA YANGA NI HUYU HAPA…JAMAA ANAJUA MNOO..

BAADA YA OKRAH…ANAYEFUATIA KUTAMBULISHWA YANGA NI HUYU HAPA…JAMAA ANAJUA MNOO..

Habari za Yanga

BAADA ya kutambulisha usajili wao mpya kiungo mshambuliaji mpya, Augustine Okrah, uongozi wa Yanga umesema hawajafunga usajili, badala yake wanatarajia kumtangaza mchezaji mwingine anayecheza nafasi ya ushambuliaji.

Ingawa uongozi haukutaja jina la mshambuliaji hiyo, lakini habari za chanzo kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa ni Leonel Ateba kutoka klabu ya Dynamo Dougla ya Cameroon ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili, na kwa sasa yuko kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa kujianda na fainali za AFCON, mwaka huu nchini Ivory Coast.

Katika kikosi cha Yanga viungo wanaongoza katika kufumania nyavu , Stephane Aziz Ki ndiye anaongoza kwa mabao ndani ya Ligi Kuu Bara akifunga 10, akifuatiwa na Maxi Nzengeli (7), kisha Pacome Zouzoua (4). Kwa upande wa washambuliaji, Kennedy Musonda amefunga matatu, Hafiz Konkoni (1) na Clement Mzize (1).

Usajili wa Ateba ni kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye safu hiyo na anakuja kuchukuwa nafasi ya Hafiz Konkoni ambaye ameshindwa kukata kiu ya Wanajagwani ambao waliamini anakuja kuchukuwa nafasi ya Fiston Mayele.

Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema baada ya kufanikiwa kumtambulisha Okrah, kazi bado inaendelea na wanaleta mtu hatari eneo la mshambuliaji ambaye anakuja kuimarisha safu hiyo.

Amesema miaka yote wanafanya usajili lakinj msimu huu wanafanya usajili bora kwa sababu wanakuja wachezaji hatari hasa kwenye safu ya ushambuliaji ambaye anakuja kuongeza zile bao tano.

“Tumemtambulisha Okrah ambaye hatutaki kumpa presha tunaacha miguu yake iongee , lakini hatutaishia kwa huyo Rais wa Yanga, Hersi Said ameniambia kuna kifaa kingine kinatua nchini.

Huyo ni mtu hatari sana kwa sababu safari hii tunaleta mfumania nyavu, timu pinzani wanatakiwa kujiandaa maana huyo anayekuja safari hii kazi yake ni kufunga tu,” amesema Kamwe.

Kuhusu usajili Kocha Mkuu wa Yanga , Miguel Gamondi amesema walifanya skauti ya kutafuta wachezaji kulingana na mahitaji yao kwa miezi miwili iliyopita pamoja na walikuwa wachezaji wengi.

“Okrah ni mchezaji mzuri ameshawahi kucheza hapa Tanzania ataomgeza kitu kwenye kikosi changu namkaribisha sana,” amesema Gamondi

SOMA NA HII  BAADA YA OKWA NA AKPAN KUTUA IHEFU...KATWILA ASHINDWA KUJIZUIA...AIBUKA NA JIPYA HILI...