Home Habari za michezo TANZIA: KIPA TAIFA STARS AFARIKI DUNIA…KUMBE ALIKUWA AFISA MKUBWA TRA

TANZIA: KIPA TAIFA STARS AFARIKI DUNIA…KUMBE ALIKUWA AFISA MKUBWA TRA

TANZIA: KIPA TAIFA STARS AFARIKI DUNIA...KUMBE ALIKUWA AFISA MKUBWA TRA

Aliyekuwa kipa wa Cosmopolitan, mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania mwaka 1967, Mohamed Mfaume ‘Difu’ (katikati) amefariki dunia Ijumaa ya Aprili 14 Jijini Dar es Salaam.

Kipa wa timu ya taifa ya Tanzania pia kuanzia miaka ya 1960 hadi 1970 mwanzoni anatarajiwa kuzikwa makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Mfaume Difu alikuwa kipa wa Cosmopolitan wakati inachukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania mwaka 1967, kabla ya kuifikisha Bara Fainali ya Kombe la Challenge mwaka 1970 ambako ilifungwa na Uganda.

Mohamed Mfaume ‘Difu’ pia alikuwa mmoja kati ya wanasoka wasomi nchini ambaye alikuwa Afisa mkubwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mungu ampumzishe kwa amani mlinda mlango Mohamed Mfaume. ‘Difu’. Amin

SOMA NA HII  YANGA WAMSHUTUKIA METACHA....WAMPIGA MARUFUKU KUNYWA POMBE...KUKATWA MIL 1....