Home CAF CAF YATUMBUA MAJIPU…WAAMUZI HAWA WANNE WASIMAMISHWA KAZI

CAF YATUMBUA MAJIPU…WAAMUZI HAWA WANNE WASIMAMISHWA KAZI

CAF YATUMBUA MAJIPU...WAAMUZI HAWA WANNE WASIMAMISHWA. KAZI

Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), imewasimamisha Waamuzi wanne wa Botswana waliochezesha mchezo wa mwisho wa kufuzu AFCON 2023 kati ya Benin dhidi ya Rwanda uliochezwa mnamo Machi 22 2023 kwa usimamizi mbovu wa mechi.

Waamuzi hao ni

JOSHUA BONDO,

MOGOMOTSI MORAKILE,

KITSO SIBANDAΒ 

TSHEPO MOKANI GOBAGOBA

Walishindwa kufuatilia ripoti zisizo sahihi kuhusu mfumo wa Usimamizi wa Mashindano (CMS) katika mchezo huo.

Kufuatia maamuzi hayo Mwamuzi wa kati Bondo amefungiwa miezi 6 huku waamuzi wasaidizi wakipewa adhabu ya kufungiwa kwa miezi 3 bila kufanya kazi kuanzia tarehe 10 Aprili 2023 kufuatia usimamizi huo unaotajwa kuwa sio wa kukubalika.

Kutokana na adhabu hiyo iliyotolewa na CAF, BFA inayozingatia maadili na uadilifu katika soka, imeamua kuwasimamisha kazi mara moja maafisa wanaohusika na upangaji wa mechi za ndani hadi itakapotangazwa tena Wakati huo huo, uchunguzi wa ndani wa nidhamu utaanza.

SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI WA YANGA ATUA AL NASSAR YA RONALDO