Home Uncategorized BOSI SIMBA ATUMA UJUMBE KWA KOCHA, WACHEZAJI KISA YANGA

BOSI SIMBA ATUMA UJUMBE KWA KOCHA, WACHEZAJI KISA YANGA

KUELEKEA kwenye mchezo kati ya Yanga na Simba utakaopigwa Machi 8, Uwanja wa Taifa, Mwenyekiti wa Bodi ya Uwekezaji ndani ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ amewatumia ujumbe wachezaji na Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck.

Mchezo huo utakuwa ni wa pili msimu huu 2019/20 baada ya ule wa kwanza uliochezwa Januari 4,2020 timu zote kutoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Kupitia Ukurasa wake wa Istagram Mo Dewji ameandika:-“Hongera Kocha Sven kwa kazi nzuri kwa kweli wachezaji wetu wanajituma kwenye michezo yote tunayocheza. Sasa tujipange kwa mchezo wa Jumapili na watani wetu. Lengo letu ni kuwa Mabingwa.

SOMA NA HII  ISHU YA DICKSON JOB WA YANGA, MTIBWA INAMALIZWA NAMNA HII