Home Habari za michezo KUMBUKIZI HIZI ZA DABI YA WATANI WA JADI…ZAIBEBA SIMBA WAZI WAZI

KUMBUKIZI HIZI ZA DABI YA WATANI WA JADI…ZAIBEBA SIMBA WAZI WAZI

KIBADENI AWACHANA MASTAA WAZAWA SIMBA...

Simba na Yanga zinakutana kwa mara ya 110 kwenye Ligi Kuu wikiendi hii tangu Jumatatu ya Juni 7, 1965.

Yanga ilishinda bao 1-0 kwenye mechi ile ya kwanza lililofungwa na Mawazo Shomvi dakika ya 15.

Rekodi zinaonyesha timu hizo zimekutana mara nyingi zaidi (59) siku ya Jumamosi katika dabi 109 walizocheza, Jumatatu zimekutana mara tatu na Jumanne mara mbili.

Lakini, Jumatano timu hizo zimekutana mara saba, Alhamisi mara mbili, Ijumaa mara moja na Jumapili zimekutana mara 35 na hata mchezo uliopita zilipotoka sare ya bao 1-1 ulipigwa pia siku ya Jumapili.

Katika michezo hiyo 35 ya Jumapili, Simba imeshinda michezo tisa, ikipoteza michezo saba na sare 19, kuonyesha kuwa ni siku ambayo imekuwa na bahati kwao kulinganisha na Yanga.

Hata hivyo Yanga ndio timu ya kwanza kushinda mchezo wa Jumapili baada ya kuichapa Simba bao 1-0 Juni 18,1972 bao lililofungwa na Leonard Chitete.

Katika michezo 35 michezo minne ilichezwa nje ya Dar es Salaam, ambapo dabi ya kwanza ilipigwa Septemba 30, 2001 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 bao la Joseph Kaniki (Simba) na Sekilojo Chambua wa Yanga.

Dabi ya pili nje ya Dar es Salaam ilichezwa Aprili 17, 2005 na Simba kushinda 2-1 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro mabao ya Simba yakifungwa na Nurdin Msiga pamoja na Athumani Machupa huku lile la Yanga akifunga, Aaron Nyanda. Mchezo wa tatu ulichezwa Agosti 21, 2005 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na Simba kushinda 2-0 mabao yakiwekwa kambani na Nico Nyagawa dakika ya 22 na 56.

Kipute cha mwisho cha dabi cha Ligi Kuu kuchezwa nje ya Dar es Salaam ilikuwa Julai 8, 2007 wakati timu hizo zikigawana alama baada ya sare ya bao 1-1 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu timu hizo kukutana Uwanja wa Taifa (Mkapa) ilikuwa Oktoba 26, 2008 na Simba kupoteza kwa bao 1-0 lililofungwa na Ben Mwalala dakika ya 15.

Katika michezo 35 Simba imekuwa mwenyeji michezo 20 wakati Yanga ikiwa mwenyeji michezo 15 na mchezo huu Simba ndio mwenyeji kwa mara nyingine. Moja ya dabi inayokumbukwa zaidi ni pamoja na ile ya Jumapili ya Mei 6, 2012 Simba ikishinda 5-0 kwa mabao ya Emmanuel Okwi aliyefunga mawili, Patrick Mafisango, Juma Kaseja na Felix Sunzu.

Miamba hawa wamekutana mara 12 ndani ya Aprili kuanzia mwaka 1965 lakini kati ya hizo sita zimekutana Jumapili huku Simba ikishinda mara mbili, sare tatu na ikipoteza mara moja.

SOMA NA HII  A-Z JINSI YANGA WALIVYOICHAKATA COASTA UNION JANA....MAYELE ATETEMA KWA HASIRA...CHICO KAONA MWEZI....