Home Habari za michezo CEO MPYA SINGIDA FOUNTAIN GATE AANZA NA MKWARA HUU…JAMAA NI KAMA SENZO...

CEO MPYA SINGIDA FOUNTAIN GATE AANZA NA MKWARA HUU…JAMAA NI KAMA SENZO KABISA YANI..

CEO Mpya Singida Fountain Gate FC

MTENDAJI Mkuu wa Singida Fountain Gate FC zamani ilikuwa inaitwa Singida Big Stars Olebile Sikwane ameweka wazi kuwa uzoefu wa kuwa kwenye maisha ya soka unampa nguvu ya kufanya vizuri kwenye timu hiyo.

Juni 14 2023 taarifa mpya ilikuwa wazi kuwa hisa za Singida Big Stars zimeuzwa kwa mmiliki wa Fountain Gate huku miongoni mwa masharti ikiwa ni kuhakikisha kwenye jina la timu mpya neno Singida halikosekani na makao makuu yatakuwa Singida.

Sikwane ambaye ni mzaliwa wa Botswana, raia wa Afrika Kusini ana uzoefu wa kufanya kazi kwenye Shirikisho la Soka la Botswana kama Mkuu wa Mashindano na Utoaji Leseni za Klabu.

Pia ameitumikia Gaborone United SC kama Meneja Mkuu uwezo wake sasa unahamia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara iliyogota ukingoni Juni 9 2023 huku mabingwa wakiwa ni Yanga.

Kiongozi huyo amesema:”Nina uzoefu na soka la Afrika na ninafurahi kuwa ndani ya Singida Big Stars imani yangu ni kupata ushirikiano na kufanya yote kwa mpango kazi mzuri.

“Kila kitu nina amini kitakuwa sawa kwa kuwa tutashirikiana na kila idara kufikia malengo ya timu yetu hii,” amesema.

Rais wa Klabu ya Singida Fountain Gate FC, Japhet Makau, amemkabidhi fulana ya Singida Big Stars (sasa Singida Fountain Gate) CEO Sikwane, wakati wa utambulisho kwa Wanahabari Juni 14.

SOMA NA HII  REKODI ZA KOCHA MPYA SIMBA SIO POA...KAMFUNDISHA RONALDO MADRID..KASHINDA LIGI YA MABINGWA ULAYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here