Home Azam FC MCHEZAJI AZAM FC KUSAJILIWA NA LIVERPOOL YA UIENGEREZA…MCHONGO MZIMA UKO HIVI

MCHEZAJI AZAM FC KUSAJILIWA NA LIVERPOOL YA UIENGEREZA…MCHONGO MZIMA UKO HIVI


KIUNGO kinda wa Azam FC, Khelffin Hamdoun, amefanikiwa kufuzu majaribio katika timu ya vijana ya Liverpool.

Hamdoun alienda mjini Liverpool, England mwezi uliopita ambapo alifanya majaribio na kufanikiwa kufaulu lakini ilishindikana kuingizwa kwenye usajili kutokana na dirisha kufungwa.

Kwa sasa bado yuko Liverpool na muda wowote kuanzia sasa anatarajia kurejea Bongo kujiunga na Azam.

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria, amesema kuwa: “Ni kweli Khelffin yupo Liverpool kwa ajili ya majaribio, ameweza kupita lakini shida imekuja usajili wa Liverpool umeshafungwa.

“Atarejea nyumbani mpaka usajili wa dirisha dogo utakapofunguliwa, Inshaallah ataenda tena.”

SOMA NA HII  WAKATI FEI TOTO AKIENDELEA 'KUKAZA SHINGO' KWA YANGA...SERIKALI WAINGILIA KATI...WATOA MSIMAMO HUU..