Home Habari za michezo BAADA YA KUMALIZA MSIMU MIKONO MITUPU…HIVI NDIVYO CHAMA ‘ANAVYOKICHAFUA’ PALE SIMBA SC…

BAADA YA KUMALIZA MSIMU MIKONO MITUPU…HIVI NDIVYO CHAMA ‘ANAVYOKICHAFUA’ PALE SIMBA SC…

Habari za Simba SC

Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama ndani ya Simba akiwa ni kinara wa kutengeneza pasi za mwisho kagawanyika vipandevipande kutokana na muda wote kuwa na makali kwenye kutengeneza pasi za mwisho.

Rekodi zinaonyesha kuwa kwenye pasi 14 ambazo ametoa ndani ya ligi kila kipindi alitoa nusu ya pasi zinazomfanya awe amegawanyika vipandevipande kila kipindi jambo linalowaogezea ugumu mabeki kumzuia.

Katoa pasi 7 kipindi cha kwanza na nyingine kipindi cha pili ambapo zile za kipindi cha kwanza ilikuwa dakika ya 14, 17, 35, 43, 10, 8, 20 na zile za kipindi cha pili ikiwa ni dakika ya 61, 53, 53, 47, 89, 60, 73

Pasi yake ya kwanza msimu huu alitoa Uwanja wa Mkapa dakika ya 61 ilikuwa dhidi ya Geita Gold, pasi ya pili ilikuwa Uwanja wa Mkapa dakika ya 14 dhidi ya Yanga, pasi yake ya tatu na ya nne ilikuwa Uwanja wa Mkapa dakika ya 17 na 35 dhidi ya Ruvu Shooting.

Tano na sita ilikuwa Uwanja wa Ushirika, Moshi dhidi ya Polisi Tanzania dakika ya 43 na 53 ngoma ilifika saba Uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Coastal Union dakika ya 53 pasi yake ya nane na tisa ilikuwa Uwanja wa Kirumba dakika ya 47 na 89 dhidi ya Geita Gold,pasi ya 10 ilikuwa dhidi ya KMC dakika ya 73.

Pasi ya 11 alitoa dakika ya 60 mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Mkapa pasi ya 12 ilikuwa dakika ya 10 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mkapa.

Ile ya 13 na 14 alitoa dhidi ya Singida Big Stars dakika ya 8 na 20 Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  TAARIFA ZA NDANI....SIMBA WARIDHIA KUMKATA WAWA...SHIBOUB APEWA MKATABA..PABLO AKUNWA...