Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA NYONI KUTEMWA SIMBA….MBRAZILI KAMTAZAMA WEE…KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HILI..

KUHUSU ISHU YA NYONI KUTEMWA SIMBA….MBRAZILI KAMTAZAMA WEE…KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HILI..

Habari za Simba SC

Uwezo mkubwa na namna anavyobeba majukumu kiraka wa Simba SC, Erasto Nyoni anapokuwa uwanjani, umeelezwa kumrahisishia kazi ya upangaji wa kikosi kocha wa timu hiyo, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, huku akisema ni mchezaji muhimu Simba.

Akizungumza nasi juu ya mchezaji huyo mkongwe, Robertinho alitaja vitu vinne vinavyomfanya aone umuhimu wa Nyoni kuwepo kikosini, kwamba kuweza kuziba mapengo ya wachezaji wengine wanapokosekana, uzoefu wake unaosaidia chipukizi kujifunza kwake, mtazamo wake na nidhamu.

Robertinho alikiri kutoumiza kichwa kumtumia Nyoni kwenye nafasi anazocheza na amekuwa akiyafanya majukumu kikamilifu, hivyo anaona ana faida kuwepo na mchezaji wa namna hiyo kikosini.

“Nyoni anajitambua na anatekeleza majukumu yake kwa usahihi, inakuwa rahisi kumfikiria kumtumia wakati wowote anapohitajika, aina ya wachezaji wa aina yake ni muhimu kwenye timu.

“Ana nidhamu ya juu, kuanzia kwenye kazi zake, mchezaji wa namna hiyo ni rahisi kukaa kwenye ramani ya kazi yake, anajua afanye nini na kwa wakati gani.” alisema kocha huyo.

Alisisitiza kuwa Nyoni ni mchezaji muhimu kwa Simba kutokana na nafasi anazocheza, hivyo anaheshimu uwezo wake na anavyochukulia vitu kwa mtazamo chanya wenye manufaa kwa klabu.

“Naangalia zaidi anachokifanya uwanjani bila kujali anaanza kikosi cha kwanza ama anaingia kipindi cha pili, kikubwa ni utekelezaji wa majukumu yake kwa usahihi na maarifa makubwa.

“Namuelezea kwasababu uzoefu wake, sina maana wengine hawawajibiki, ila lipo jambo muhimu la kujifunza kwa chipukizi ili kufanya kazi zao kwa kiwango cha juu,” alisema. Ukiachana na kocha, Meneja wa zamani wa Azam FC, Philipo Alando alisema Nyoni ana nidhamu ya kazi inayomfanya hadi sasa aendelee kucheza soka la ushindani.

“Soka linahitaji nidhamu kubwa, halina konakona, hivyo Nyoni anaonyesha kwa vitendo namna anavyotekeleza majukumu yake, anapaswa kupewa heshima inayostahili.”

SOMA NA HII  SIMBA: MTIBWA SUGAR HUWA WANATUPA CHANGAMOTO,