Home Simba SC AL MERRIKH WALIA KUHUJUMIWA, WACHEZAJI NANE WAKUTWA NA CORONA

AL MERRIKH WALIA KUHUJUMIWA, WACHEZAJI NANE WAKUTWA NA CORONA

 


IMERIPOTIWA kuwa wachezaji 8 wa kikosi cha Al Merrikh ya Sudan ambayo leo Machi 16 itacheza na Klabu ya Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wamekutwa na Virusi vya Corona. 

Kupitia ukurasa rasmi wa Istagram wa Al Merrikh umeripoti kuwa wanaamini ni mpango wa kuwadhoofisha ambao umechezwa jambo ambalo limewafanya wapeleke file hilo mbele Umoja wa Afrika, (AU).  

Taarifa zinaeleza kuwa wamepewa matokeo hayo saa moja kabla ya mchezo wa leo ambao unachezwa Uwanja wa Mkapa.

Miongoni mwa wachezaji ambao wametajwa kuwa na Corona ni Abdul Rahman Karngou, Altaj Yaqoub, Bhakit Khamis, Ramadan Ajab, Tony, Bakir Al Madina, Saif Al-Damazin, Emad Abdul-Manim.


SOMA NA HII  PAMOJA NA KUTAMBULISHWA ....KOCHA MPYA SIMBA KUTUA MISRI...AHMED ALLY AFICHUA MPANGO WOTE ULIVYO...