Home Uncategorized WACHEZAJI WAPEWA SOMO HILI LA KUFANYA WAKATI HUU BAADA YA KAMBI KUVUNJWA

WACHEZAJI WAPEWA SOMO HILI LA KUFANYA WAKATI HUU BAADA YA KAMBI KUVUNJWA

NADIR Haroub, Meneja wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amewataka wachezaji kuendelea kufanya mazoezi kipindi hiki cha mapumziko ya dharula kwa ajili ya kujikinga na kusambaa kwa virusi vya Corona.

Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili, Ligi ya Wanawake, Ligi ya Mabingwa wa Mkoa, Umitashumta na shughuli zote za kimichezo zimesimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja na Serikali kutokana na kupambana na kusambaa kwa Virusi vya Corona.

Haroub amesema :”Kipindi hiki cha mapumziko kwa wachezaji ambayo ni maalumu kwa ajili ya kupambana na kusambaa kwa Corona ni lazima wachezaji kujilinda afya zao na kufuata kanuni za afya, wasisahau pia kufanya mazoezi.

“Ni muhimu kwa wachezaji kufanya mazoezi kwani ndio asili yao iwapo watashindwa kufanya hivyo itawarudisha nyuma kwenye uwezo wao,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE