Home Uncategorized POCHETTINO: LAUTARO MARTINEZ NI MSHAMBULIAJI BORA DUNIANI

POCHETTINO: LAUTARO MARTINEZ NI MSHAMBULIAJI BORA DUNIANI


ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Tottenham, Mauricio Pochettino amesema kuwa nyota anayekipiga ndani ya Inter Milan, Lautaro Martinez ni miongoni mwa washambuliaji wazuri dunaini kutokana na ubora wake ndani ya uwanja.

Nyota huyo mwenye miaka 22 yupo chini ya Antonio Conte na kwa msimu huu wa 2019/20 ametupia mabao 16 na kutengeneza pasi nne za mabao katika mechi 31 ambazo amecheza.
Uwezo wake kwa sasa umeonekana kuwavutia Barcelona ambao wanahitaji kuinasa saini yake kwa sasa ili kumpeleka ndani ya La Liga.
Pochenttino amekuwa nje bila kazi baada ya kupigwa chini na Spurs mwezi Novemba amesema anaelewa thamani ya Martinez na akipewa nafasi ndani ya Barcelona atafanya mambo makubwa.
‘Lautaro Martinez ni miongoni mwa wachezaji wazuri duniani hasa kwa nafasi yake ya ushambuliaji ambayo anaicheza kwa sasa, sio kwa ajili ya kile anachokifanya kwa sasa bali kwa malengo yake ya baadaye anazidi kuwa bora kila iitwapo leo,” amesema.

Miongoni mwa klabu ambazo pia zinahusishwa kuinasa saini yake ni pamoja na Chelsea iliyo chini ya Kocha Mkuu Frank Lampard, dili lake limebakiza miaka mitatu ndani ya Inter Milan na amekuwa na pacha nzuri na nyota mwenzake  Romelu Lukaku.
SOMA NA HII  SIMBA YAPIGA MATIZI LEO UWANJA WA SOKOINE, MBEYA