Home Uncategorized LUSAJO BANA, APATA KIGUGUMIZI KUZUNGUMZIA DILI LAKE LA YANGA

LUSAJO BANA, APATA KIGUGUMIZI KUZUNGUMZIA DILI LAKE LA YANGA


RELLIANTS Lusajo, mshambuliaji namba moja wa Klabu ya Namungo FC amesema kuwa hawezi kuzungumzia juu ya dili lake la kutua ndani ya Klabu ya Simba ama Yanga kwa sasa kwa kuwa bado ana mkataba kwenye klabu yake.

Lusajo inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za mabosi wake wa zamani Yanga ambao wanahitaji saini yake huku Simba pia wakiiwinda saini yake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Lusajo amesema:”Nina mkataba na Namungo kwa sasa siwezi kuzungumza kuhusu ishu ya kwenda Yanga ama Simba.

“Ni kweli mkataba wangu upo karibu kuisha ila haina maana kwamba ndio nishajua kuwa wapi nitasaini hapana, nangoja mkataba uishe kwanza,” amesema Lusajo.

Lusajo ametupia mabao 11 ndani ya Namungo FC inayofundishwa na Hitimana Thiery.

SOMA NA HII  SASA MECHI KUPIGWA KAMA KAWAIDA, NYUMBANI NA UGENINI, VITUO HAKUNA