Home Uncategorized ARUSHA FC YAIANGUKIA TFF NA WADAU, HALI NI TETE

ARUSHA FC YAIANGUKIA TFF NA WADAU, HALI NI TETE


UONGOZI wa Arusha FC, inayoshiriki Ligi Dajaja la Kwanza umeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuzitazama timu zote zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza pamoja na zile za madaraja ya chini ili kuwapa sapoti ya kuweza kumalizia mechi zilizobaki kutokana na kuyumba kiuchumi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa AFC, Bahati Msilu amesema kuwa klabu nyingi zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza hazina wadhamini ni mali ya mashabiki  jambo linalowafanya wawe kwenye wakati mgumu kumaliza mechi zao iwapo ligi itarejea.

“Tulikuwa tumepanga bajeti ya kumaliza ligi ambapo mechi zetu nne bajeti yetu ilikuwa milioni 14 kibindoni baada ya shughuli kusimama mambo mengi kwetu pia yalisimama hakuna fedha.

“Kikubwa ambacho ninakiomba kutoka kwa TFF waangalie namna ya kuweza kutupa sapoti iwe kwa fedha kwa ajili ya kumalizia mechi hizi maana tumefurahia tamko la Rais John Magufuli kufikiria kwamba ligi inaweza kurudi hivi karibuni,” amesema.

Ligi zote zilisisimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo ilisimamishwa Machi 17 na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

SOMA NA HII  MAGUIRE, POGBA KUIVAA CHELSEA JUMAPILI