Home Uncategorized MOLINGA NA EYMAEL WAFIKA KANDA YA ZIWA

MOLINGA NA EYMAEL WAFIKA KANDA YA ZIWA


KOCHA Mkuu wa Yanga na mshambuliaji namba moja wa Yanga kwa sasa wametia timu Mwanza ikiwa ni safari yao ya kuelekea Shinyanga.

Safari yao imeanza leo Dar kwa ndege ambapo wataungana na wachezaji waliotangulia kwa basi Juni 10.

Eymael alichelewa kujiunga na timu kwa kuwa alikuwa nchini Ubelgiji ambapo alikwenda baada ya mapumziko ya lazima yaliyosababishwa na Corona na inaelezwa kuwa alikwenda kukamilisha masuala ya ndoa.

Molinga hakuwa kwenye msafara wa kwanza kwa kile kilichoelezwa kuwa hakujumuishwa kwenye kikosi kitakachosafiri.

Yanga itamenyana na Mwadui FC kesho, Juni 13 ikiwa ni mchezo wa ligi Uwanja wa Kambarage.
SOMA NA HII  KMC WAIWAHI MAPEMA TP MAZEMBE