Home Uncategorized UJUMBE WA RUVU SHOOTING HUU HAPA

UJUMBE WA RUVU SHOOTING HUU HAPA

UONGOZI wa Ruvu Shooting, umesema kuwa upo tayari kwa michezo yote iliyobaki kusepa na pointi tatu muhimu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa morali ya wachezaji ni kubwa na kila mmoja yupo tayari kuona timu inapata ushindi.

“Wachezaji wapo tayari, kila mmoja anatambua jukumu lake hivyo nina amini mwendelezo wa kupapasa utakuwa kama ilivyokuwa kawaida bila mashaka yoyote,” amesema.

Ruvu Shooting ipo nafasi ya 11 ikiwana pointi 39 baada ya kucheza mechi 28.Juni 14 itashusha kete yake mbele ya Simba Uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  ANAANDIKA HAJI MANARA AKIWAOMBA WATANZANIA WAMPE JAPO HESHIMA