Home Uncategorized MOROCCO KUMSAKA MBADALA WA ADAM SALAMBA

MOROCCO KUMSAKA MBADALA WA ADAM SALAMBA


 HEMED Morroco, Kocha Mkuu wa Klabu ya Namungo FC amesema kuwa ataongeza washambuliaji wa kimataifa kwenye timu yake ili kuongeza nguvu ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika.


Jana iliweza kutinga hatua ya nne ya Kombe la Shirikisho baada ya kushinda mabao 2-0 dhidi ya Green Warriors kwenye mchezo wa hatua ya tatu uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mabao ya Namungo yalipachikwa na Idd Kipagwile kwa mpira wa adhabu nje ya 18 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa faulo ilikuwa dakika ya 8 kwa pigo huru na Sixtus Sabilo dakika 78.

Morroco amesema:”Ninahitaji kuongeza washambuliaji hasa ukizingatia kwamba mchezaji wetu mmoja bado anasumbuliwa na majeraha na hajarejea kwenye ubora.


“Adam Salamba bado hayupo fiti hivyo ni wakati wetu kuingia sokoni kusaka mshambuliaji ambaye tutakuwa naye ndani ya kikosi kwani mbali na ligi tunashiriki mashindano ya kimataifa,” .

Namungo FC ina kazi ya kusaka ushindi na kuulinda ule wa mabao 2-0 walioupata Uwanja wa Azam Complex Desemba 23 kwenye mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa kati ya Januari 5-6 nchini Sudan.

SOMA NA HII  UBINGWA WA LIVERPOOL MASHAKANI IWAPO MSIMU WA 2019/20 UTAFUTWA