Home Uncategorized BEKI SIMBA MALI YA KAGERA SUGAR

BEKI SIMBA MALI YA KAGERA SUGAR

 


YUSUPH Mlipili aliyekuwa beki wa kikosi cha Simba amesaini dili la mwaka mmoja kukitumikia kikosi cha Kagera Sugar kinachonolewa na Kocha Mkuu, Mecky Maxime.


Mlipili aliachwa na Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandebroeck msimu wa 2020/21 kutokana na kukosa namba ndani ya kikosi hicho.

Nafasi yake ilichukuliwa na ingizo jipya Kened Juma ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Singida United ambayo imeshushwa madaraja mawili kwa sasa.

Huu ni usajili wa kwanza kwa Kagera Sugar kwenye dirisha dogo ambalo limefunguliwa Desemba 16 na linatarajiwa kufungwa Januari 15,2021.

Mlipili ni miongoni mwa wazawa ambao waliweza kufanya vizuri ndani ya Simba zama za Patrick Aussems ambaye alikuwa akipenda kuwaanzisha na pacha wake Erasto Nyoni ambaye ni mkongwe.
Kabla ya kuibukia Kagera Sugar ambapo anaungana na mtambo wa mabao, David Luhende mwenye pasi tano na bao moja alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya Coastal Union ya Juma Mgunda.
SOMA NA HII  KIBANO KIZIMA CHA SIMBA MBELE YA MTIBWA SUGAR KILIKWENDA KWA MWENDO HUU