Home Uncategorized KIBANO KIZIMA CHA SIMBA MBELE YA MTIBWA SUGAR KILIKWENDA KWA MWENDO HUU

KIBANO KIZIMA CHA SIMBA MBELE YA MTIBWA SUGAR KILIKWENDA KWA MWENDO HUU

 


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, jana walibanwa mbavu mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wao wa pili mzunguko wa pili kwa kufungana bao 1-1.

Simba walikuwa wa kwanza kucheka na nyavu dakika ya 44 kupitia kwa kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Mzamiru Yassin baada ya kiungo Baraka Majogoro kufanya makosa nje kidogo ya 18 ambapo baada ya kufunga bao hilo kiungo huyo mzawa aliwaomba msamaha mashabiki wa Mtibwa Sugar

 Bao hilo la Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck liliwekwa sawa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro dakika ya 46 kwa kichwa kilichofungwa na Boban Zingiratius katikati yam situ wa mabeki wa Simba akimalizia pasi ya Issa Rashid baada ya mlinda mlango Aishi Manula kuacha lango wazi.

Jitihada za Simba kusaka pointi tatu na Mtibwa Sugar kulipa kisasi cha mchezo wao wa mwisho msimu uliopita kwa kufungwa mabao 3-0 na Simba Uwanja wa Jamhuri ziligonga mwamba.

Mikono ya Abubakari Twalib, mlinda mlango wa Mtibwa Sugar iliweza kuokoa hatari za nyota wa Simba waliokuwa wakiongozwa na John Bocco ikiwa ni pamoja na ile iliyopigwa dakika ya 24 na Clatous Chama,dakika ya 31 kupitia kwa Bocco, dakika ya 34 kupitia kwa Jonas Mkude na Joash Onyango dakika ya 42 kichwa chake kiligonga mwamba,Luis Miqussone dakika ya 83.

Mikono ya Manula nayo ilikutana na balaa ambapo dakika 27, Juma Nyangi alipita katikati ya msitu wa mabeki wa Simba na kuachia shuti kali ambalo liliokolewa,Ibrahim Hamad Ibrahim naye alifanya jaribio kali dakika ya 29 ila alikosa na jaribio kali kwa Mtibwa Sugar lilifanywa dakika ya 85 na Jaffary Kibaya likaokolewa na Manula.

Mtibwa Sugar inalazimisha sare ya pili ikiwa nyumbani baada ya mchezo wa kwanza kulazimisha sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting Uwanja wa Gairo na jana ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Simba.

SOMA NA HII  COASTAL UNION YAZITAKA POINTI TATU ZA NAMUNGO