Home Uncategorized COASTAL UNION YAZITAKA POINTI TATU ZA NAMUNGO

COASTAL UNION YAZITAKA POINTI TATU ZA NAMUNGO

KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa kesho, Juni 13 itakuwa ni kazi moja tu kuendelea pale walipoishia kwenye mechi za ligi kwa kusaka pointi tatu mbele ya Namungo FC.

Coastal Union itamenyana na Namungo Uwanja wa Mkwakwani Tanga mchezo wa ligi utakaochezwa majira ya saa 10:00 jioni.

Mgunda amesema:”Hatukuwa kwenye ushindani kwa muda mrefu ila ni muhimu kuendelea pale ambapo tuliishia ili kuona namna gani tutaendelea kuwa bora.

“Wapinzani wetu ni timu imara ila hakuna namna nasi pia tupo imara kutafuta ushindi,”

SOMA NA HII  BREAKING NEWS!! KAGERA SUGAR YASALIA LIGI KUU, MWADUI NAYO YACHEKELA DHIDI YA GEITA