Home Simba SC HIVI NDIVYO BOCCO,MUGALU NA KAGERE WALIVYOHUSIKA KATIKA MAGOLI 46 YA SIMBA

HIVI NDIVYO BOCCO,MUGALU NA KAGERE WALIVYOHUSIKA KATIKA MAGOLI 46 YA SIMBA


MASTRAIKA watatu wa kikosi cha Simba wamefunga mabao 22, kati ya 46 ambayo yamefungwa na kikosi kizima mpaka sasa katika Ligi Kuu Bara.

Mastraika hao nahodha, John Bocco na Meddie Kagere ambao ndio vinara wa ufungaji kila mmoja akifunga mabao tisa wakati Chriss Mugalu nae ameweka kambani manne.

Kutokana na ushindani huo wa kufunga mabao katika ligi mfungaji bora wa msimu uliopita, Kagere anasema yameongeza makali yake katika zoezi la kufunga msimu huu.

Kagere anasema katika msimu huu bado hajawa anapewa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza mara kwa mara kutokana na ushindani wa namba uliokuwepo katika kikosi hicho.

“Licha ya changamoto hiyo ya kucheza ambayo nimekutana nayo malengo yangu ya msimu huu ni kuisaidia timu kufikia mafanikio kama kutetea ubingwa wa ligi,” anasema.

“Majukumu ya nafasi yangu uwanjani ni kufunga kwa maana hiyo msimu huu natamani kufikia idadi ya mabao ambayo nilimaliza nayo ligi msimu uliopita na baada ya hapo ndio nitakuwa na malengo ya mengine baada ya kufikia hayo,” anasema Kagere.

Katika msimu uliopita Kagere alimaliza kama mfungaji bora wa ligi akiwa amefunga mabao 22, wakati msimu mmoja nyuma alichukua tuzo hiyo akimaliza na mabao 23.

SOMA NA HII  SAA CHACHE KABLA YA MECHI..KAPOMBE AIBUKA NA JAMBO SIMBA...UONGOZI WATOA TAMKO..