Home Ligi Kuu VURUGU ZA LIGI KUU BARA NI MPAKA JULAI BADALA YA KUISHA JUNI

VURUGU ZA LIGI KUU BARA NI MPAKA JULAI BADALA YA KUISHA JUNI


 ALMAS Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) amesema kuwa msimu wa 2020/21 utakamilika Julai tofauti na awali ambapo ulitarajiwa kukamilika Juni.

Mabadiliko hayo ya muda wa ligi kukamilika yametokana na kutokea kwa msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli ambaye alitangulia mbele za haki Machi 17.

Kutokana na msiba huo ambao ni mkubwa kwa Tanzania na Afrika kiujumla kulikuwa na siku 21 za maombolze ambazo zinaendelea mpaka wakati huu na zinatarajiwa kukamilika Aprili 7.

Kasongo amesema:”Awali ligi yetu ya Tanzania Bara ilipaswa kumalizika tarehe 12 mwezi wa sita lakini kulingana na mabadiliko ligi itaisha tarehe 11 mwezi wa saba.

“Hii inatokana na kuwa na mabadiliko ambayo yamefanyika kwenye ligi kuendena na siku 21 ambazo ni za maombolezo,” .

Leo TBLB imetoa ratiba ambayo inaonyesha kwamba Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mechi za Kombe la Shirikisho zitarejea kuanzia Aprili 8.

Kwa timu ambazo zitaangukia kucheza Playoff 2020/21 zitacheza mchezo wa kwanza Julai 14 na ule wa pili utakuwa ni Julai 17 na fainali ya Kombe la Shirikisho itakuwa ni Julai 18, Kigoma huku shughuli zote zikitarajiwa kufungwa Julai 21 kwa tuzo kutoka TFF.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA MBEYA CITY