Home Simba SC GOMES – SIJUI LOKOSA YUPO WAPI

GOMES – SIJUI LOKOSA YUPO WAPI

 


KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Didier Gomes amesema kuwa hajui alipo mshambuliaji wake Lokosa Junior.

Junior raia wa Nigeria alisajiliwa na Simba kwa dili la miezi 6 na sababu kubwa ya usajili wake ni kwa ajili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akiwa ndani ya kikosi cha Simba hajaweza kuonekana kwenye mechi ya ushindani ambapo Simba ikiwa imecheza mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi hajacheza mchezo hata mmoja.

Nafasi yake ya ushambuliaji amekuwa akianza Chris Mugalu pamoja na Meddie Kagere ambaye mechi nyingi amekuwa akianzia benchi huku John Bocco taratibu akirejea kwenye ubora wake.

Katika mazoezi ya Simba ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Simba Mo Arena vilivyoppo Bunju, Lokosa hajaonekana mazoezini huku habari zikieleza kuwa amevunjiwa mkataba wake na mabosi hao wa mtaa wa Msimbazi.

Kuhusu Lokosa, Gomes amesema:”Sijui kwa kweli kuhusu huyo, ila siwezi kulizungumzia jambo hilo ila ukweli ni kwamba sijamuona muda mrefu kwenye eneo la mazoezi,” .

SOMA NA HII  ZA NDAAANII KABISA....MOSES PHIRI NA SIMBA MHHHH....