Home Uncategorized TWIGA STARS KUANZA KAZI LEO NA MAURITANIA MASHINDANO YA UNAF

TWIGA STARS KUANZA KAZI LEO NA MAURITANIA MASHINDANO YA UNAFBAKARI Shime, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania, Twiga Stars amesema kuwa watatumia nafasi ya kualikwa kwenye mashindano ya Umoja wa Wanawake kwa nchi za Kaskazini mwa Afrika (UNAF) kiukamilifu nchini Tunisia.

Twiga Stars imealikwa kwenye mashindano hayo yanayofanyika nchini Tunisia na leo itafungua pazia kwa kuanza kucheza na timu ya Mauritania majira ya saa 7:00 mchana Uwanja wa Kram.

“Wachezaji wapo vizuri na mazoezi ambayo wameyafanya yamewaweka kwenye morali nzuri ni matumaini yetu kwamba tutapata matokeo chanya kwenye mashindano haya,” amesema.

Timu shiriki kwenye mashindano haya ni pamoja na Tunisa, Morroco, Mauritania,Algeria pamoja na Tanzania.

SOMA NA HII  NYOTA WATATU STARS WAONDOLEWA NAFASI ZAO ZACHUKULIWA NA MAJEMBE HAYA