Home Habari za michezo MZIZE AFUNGUKA KUHUSU MAYELE KWENYE HILI

MZIZE AFUNGUKA KUHUSU MAYELE KWENYE HILI

Habari za Yanga SC

Mshambuliaji wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans, Clement Mzize, ametoa siri ya bao pekee alilofunga dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan kwenye mechi ya mkondo wa pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwataja, Fiston Mayele na Miguel Gamondi kuhusika.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam juzi Jumamosi (Septemba 30) na Young Africans kushinda 1-0, hivyo kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25, Mzize alitokea benchi akichukua nafasi ya Kennedy Musonda.

Mzize amesema anamshukuru aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Mayele kwani ushauri wake unampa mafanikio ambayo hakuwahi kuyatarajia.

Amesema siku zote kabla ya Mayele kuondoka Young Africans na kwenda kujiunga na Pyramids ya Misri, alikuwa akimshauri vitu vingi kimchezo kutokana na uwezo aliokuwa nao.

“Ninamshukuru Mayele, ushauri wake umenisaidia kwa kiasi kikubwa, ni mtu ambaye amenifanya niwe na historia kwenye maisha ya mpira,” amesema Mzize.

Aidha, ameshukuru kufunga magoli mawili katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Al-Merrikh Ugenini na nyumbani.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Rwanda kutokana na Sudan kuwa katika machafuko ya kisiasa, Young Africans ilishinda mabao 2-0, yakifungwa na Musonda na Mzize, hivyo kufuzu hatua ya makundi kwa jumla ya mabao 3-0.

Kuhusu Gamondi, Mzize amesema alimtaka kutumia vizuri mipira ya Krosi kwa ajili ya kupachika bao jambo ambalo alilitekeleza kwa vitendo dakika ya 66, akifunga kwa kichwa.

“Kocha aliniambia niwe makini na kutofanya makosa kwenye eneo la hatari na kutumia vizuri mipira ya krosi na nilifanikiwa kuipeleka timu hatua ya makundi.

SOMA NA HII  BANDA SASA ANATAKIWA KUONGEA LUGHA MOJA NA MBRAZIL