Home Ligi Kuu KOCHA MPYA KAGERA SUGAR KUANZA KUONGEZA MAKALI YA WASHAMBULIAJI

KOCHA MPYA KAGERA SUGAR KUANZA KUONGEZA MAKALI YA WASHAMBULIAJI


 KOCHA Mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Francis Baraza amesema kuwa kazi ya kwanza atakayoanza nayo kwa sasa ni kushughulika na safu ya ushambuliaji ili irejeshe makali yake.

Baraza amechukua mikoba ya Mecky Maxime ambaye alifutwa kazi kutokana na mwendo mbovu wa timu yake na mchezo wa mwisho kukaa benchi ilikuwa mbele ya Azam FC ambapo ubao wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 1-2 Azam FC.

Kwa sasa Maxime yupo huru ambapo amekuwa akitajwa kuibukia Biashara United kuchukua mikoba ya Baraza.

Baraza amesema kuwa amewatazama washambuliaji wake walivyo na ameona ni lazima aanze nao ili kuongeza kasi kwenye ushambuliaji.

“Ili timu ipate ushindi ni lazima ifunge na ufungaji unaanzia kwa washambuliaji pamoja na viungo ambao kazi yao ni kutengeneza nafasi za kufunga kwa washambuliaji.

“Kikubwa ambacho nina amini kwamba kinawezekana ni kupata matokeo katika mechi zetu hivyo mashabiki watupe sapoti bila kuwa na mashaka nasi,” .

Kagera Sugar kwenye msimamo ipo nafasi ya 13 ina pointi 25 baada ya kucheza mechi 24. Safu ya ushambuliaji imefunga mabao 23.

SOMA NA HII  KMC NGUVU ZOTE SASA MKWAKWANI KWA COASTAL UNION