Home Habari za michezo UHALISIA WA MANARA NA SOKA LA TANZANIA

UHALISIA WA MANARA NA SOKA LA TANZANIA

HAJI MANARA AUMBUKA...NI BAADA YA KUMGOMBANISHA RAISI YANGA NA MTANGAZAJI

Simba na Yanga walikuwa na Hajis Manara lakini kwa sasa anatumikia adhabu ya kifungo alichopewa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania “TFF”.

Mtu akiniuliza swali; “Namjua vipi HAJI MANARA nje ya kazi alizowahi kufanya kama Afisa Habari?”, nitamjibu kirahisi sana “NAMFAHAMU @hajismanara KAMA GOOGLE YA MPIRA WA TANZANIA na Ulimwengu kwa Ujumla”.

Inawezekana ikawa vigumu watu kuniamini, Yes Sijawahi kukutana nae, Kukaa wala kuongea na Manara lakini nasoma na kumsikiliza sana ni kweli naweza kumtumia kama google ya mpira wa Tanzania kama navyomtumia Pascal Kabombe kwenye baadhi ya mambo.

Manara ndio kachora mchongo mzima kuhusu kujaza viwanja, Zakazakazi nisaidie kama miaka ya nyuma kuna Afisa Habari aliwahi kuita mashabiki uwanjani na wakajaa (Full House)

Hajis Manara alikuwa ni mwanadamu wa tofauti sana alipokuwa akisisimama mbele ya Camera kuongelea mpira basi hata kama ulikuwa unafanya shughuli zako ilikuwa rahisi sana kuziacha, Katika ubunifu na namna ya kuyaendesha matamasha makubwa Haji amekuwa ni mtu hasa.

Kwa kiasi kikubwa Maafisa Habari wa sasa wa vilabu kama Simba na Yanga wanafanya vyema lakini njia na kodi zote Manara ndio alifungua, ukijaribu kukumbuka kuhusu “Do or Die” ya kwa Mkapa, “The Return of Champion”, “War in Dar” n.k. zilikuwa ni juhudi kubwa sana za Manara.

SOMA NA HII  RIVERS UNITED WAZIDIWA KETE NA YANGA...WACHACHAWA! WAPAGAWA!...ISHU NZIMA IKO HIVI