Home Simba SC MZAMIRU :- HAKUNA WAKUTUSIMAMISHA KWA TIMU ZA TANZANIA

MZAMIRU :- HAKUNA WAKUTUSIMAMISHA KWA TIMU ZA TANZANIA


KIUNGO fundi wa Klabu ya Simba asiyekuwa na madaha awapo dimbani Mzamiru Yassin amesema, hakuna timu ambayo inawatisha kuelekea kutetea kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2020/2021.

Mzamiru mchezaji ambaye ukimtizama huwezi kuyaona madhara yake ndani ya dimba kwa haraka haraka kwani ni moja ya nyota wenye utulivu wa hali ya juu wawapo katika utekelezaji wa majukumu yao ndani ya uwanja.

Amesema, wao kama wachezaji wanajua wajibu wao na kuyatimiza majukumu yao vilivyo hivyo mpaka sasa hawajaona timu ambayo inaweza kuwafanya washindwe kutetea taji hilo.

“Kwenye ligi naona mpaka sasa hakuna mtu ambayo anaweza kutuzuia kupambana katika kutetea ubingwa wetu, tumejiandaa na tunajua majukumu yetu kama wachezaji, ili kufikia malengo yetu”amesema Mzamiru.

Mzamiru mpaka sasa katika michezo aliyocheza kwenye Ligi amefanikiwa kufunga mabao mawili akitoa pasi moja akicheza faulo tano huku akitunukiwa kadi moja ya njano.

Kwenye msimamo wa timu yake inashika nafasi ya pili ikishuka dimbani mara 20 ikishinda michezo 12 sare nne na kupoteza miwili huku watani zao Yanga wakishika usukani kwa kuwazidi michezo mitatu mbele na kuwa na idadi ya pointi 50 wakishinda mechi 14 sare nane na kupoteza mmoja huku Azam FC nafasi ya tatu michezo 24 akishinda 12 sare nane na kupoteza minne na kujikusanyia pointi 44.

SOMA NA HII  RASMI : OKWI KUVAA TENA UZI WA SIMBA SC MSIMU UJAO