Home Uncategorized UNITED YASHINDA VITA YA KUMPATA NYOTA WA NIGERIA MBELE YA SPURS

UNITED YASHINDA VITA YA KUMPATA NYOTA WA NIGERIA MBELE YA SPURS


MANCHESTER United imekamilisha dili la kumpata kwa mkopo Odion Ighalo kwa dau la pauni milioni tatu.

Dili la nyota huyo halijazungumzia ishu ya kumnunua jumla endapo United watamkubali.

Ighalo anakuwa mbadala wa Marcus Rashford ambaye ndiye kinara wa kutupia ndani ya United akiwa na mabao 14 Ila anasumbuliwa na majeruhi anatarajiwa kukaa nje kwa muda wa miezi sita.

Imeelezwa kuwa vita kubwa kuipata saini yake ilikuwa inachezwa pia na Jose Mourinho wa Spurs ambaye naye alikuwa anahitaji mshambuliaji kabla dirisha la mwezi Januari halijafungwa.

Manchester United imethibitisha kuwa nyota huyo aliyekipiga Watford na alikuwa anakipiga Shanghai Shenhua atakuwa ndani ya kikosi mpaka mwisho wa msimu.

Atakuwa chini ya Ole Gunnar Solskjaer ambaye amesema kuwa Odion ni mchezaji mwenye uzoefu na uwezo ndani ya Uwanja.

Nyota huyo raia wa Nigeria, mwenye miaka 30, amefunga jumla ya mabao 46 kwenye mechi 72 alizocheza akiwa na Shanghai Shenhua.

SOMA NA HII  MEDDIE KAGERE AZUA GUMZO SIMBA, REKODI ZATAJWA