Home Simba SC RASMI : OKWI KUVAA TENA UZI WA SIMBA SC MSIMU UJAO

RASMI : OKWI KUVAA TENA UZI WA SIMBA SC MSIMU UJAO


Kama ndivyo, basi shughuli msimu ujao itakuwa pevu, Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi yu mbioni kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania, Simba Sports Club .

Okwi ambaye hivi sasa anacheza nchini Misri katika klabu ya Al Ittihad Alexandria, anatarajiwa kujiunga na Simba SC kama mchezaji huru mara baada ya mkataba wake na timu yake ya misri kuisha mwishoni mwa msimu huu.

Kujiunga kwa Okwi ndani ya Simba SC kunathibitishwa na ujumbe wa nahodha wa Simba SC, John Bocco kwenye ukurasa wa instagram wa Okwi, ambapo Bocco aliandika maneno yenye kumaanisha kuwa anamkaribisha tena Okwi kujiunga na Simba SC kwenye dirisha kubwa la usajili.

Endapo, Okwi atajiunga tena na Simba SC itakuwa ni mara ya nne kwa nyota huyo wa Uganda kujiunga na miamba ya Soka nchini.

Itakumbukwa kuwa, kwa mara ya kwanza Okwi alianza safari yake ya soka la kimataifa akiwa na Simba kwenye msimu wa 2010/11 kabla ya kuja kuuzwa nchini Tunisia kwenye klabu ya Etoile Du Sahel , Okwi alijunga tena na Simba SC msimu wa mwaka 2014/15 akiwa kama mchezaji huru, ambapo alicheza kwa msimu mmoja na kuuzwa nchini Denmark .


Okwi alijiunga na Simba SC kwa mara ya tatu msimu wa 2017/18 akitokea nchini Uganda kwenye klabu ya AS Villa, ambapo aliichezea Simba mpaka mwisho wa msimu wa na kujiunga na timu ya Al Ittihad Alexandria
 kama mchezaji huru.

Aidha akiwa na Al Ittihad Alexandria inayoshiriki ligi kuu nchini Misri, Okwi amekuwa hapati nafasi ya mara kwa mara kitu ambacho kinachochea yeye kutaka kurudi Simba SC ambapo alifanikiwa kujenga ufalme na kuaminiwa na mashabiki pamoja na viongozi wa klabu.

Akiwa na Simba SC, Okwi alifanikiwa kushinda Ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa 2017/18 na msimu wa 2018/19pamoja na kufanikiwa kuipa Simba SC nafasi ya kuingia Robo fainali ya klabu bingwa katika msimu wa 2018/19 ambapo walitolewa na TP Mazembe ya DRC Congo.

SOMA NA HII  AKILI YA SIMBA SASA NI KWA COASTAL UNION, MSUTUPANGIE KIPA LANGONI

Hata hivyo,kujiunga kwake na Simba kutaifanya timu hio, kupunguza baadhi ya wachezaji wake wa kimataifa ili kuweza kukidhi matakwa ya kikanuni ya ligi kuu, ambayo yanaitaka timu shiriki kuwa na jumla ya wachezaji kumi wa kimataifa .

Lakini pia kujiunga na Simba SC, mbali na kutaisaidia Simba kuwa na safu kali ya ushambuliaji pia kutamlazimu Okwi kuwania namba katika kikosi cha kwanza cha Kocha Didier Gomes da Rosa ambacho msimu huu kimaishia nafasi ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika kwa kutolewa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.