Home Habari za michezo AKILI YA SIMBA SASA NI KWA COASTAL UNION, MSUTUPANGIE KIPA LANGONI

AKILI YA SIMBA SASA NI KWA COASTAL UNION, MSUTUPANGIE KIPA LANGONI

KIPA CHIPUKIZI SIMBA AMWAGA SIRI NZITO...AMTAJA AISHI MANULA...ISHU IKO HIVI A-Z

Kikosi cha timu ya Simba kimerejea nchini jana Jumatatu, Septemba 18, 2023 wakitokea nchini zambia ambako walikwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Power Dynamos ambapo walitoa sare ya bao 2-2.

Akizungumza leo, Meneja wa Habari na mawasiliano wa Kalbu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kikosi hicho kimeelekea kambini moja kwa moja kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Coastal Union utakaopigwa keshokutwa Alhamisi, Septemba 21, jijini Dar es Salaam.

“Coastal Union tunawakaribisha, tulikuwa na hamu nao kweli tangu tulivyoomba tucheze mechi na wao kama wiki mbili zimepita, mambo yakawa mengi, mara wamevunja kambi.

“Kifupi ni kwamba walikula nyoya, lakini sisi ni people, tumekutana, Alhamisi tutakutana nao kwa ajili ya kwenda kuwapelekea moto Wagosi wa Kaya.

“Kuhusu kipa Ayoub Lakred, Coastal wasitupangie, anaweza akadaka kipa yeyote yule ambaye Simba SC tutamuamini,” amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  KARIA AIBWAGA SIMBA KAMA MASIHARA