Home Simba SC SIMBA: WACHEZAJI WOTE WAPO KAMILI KUIKABILI AS VITA

SIMBA: WACHEZAJI WOTE WAPO KAMILI KUIKABILI AS VITA

 


SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba amesema kuwa kesho wanahitaji kupata matokeo chanya mbele ya AS Vita.


Simba itawakaribisha AS Vita Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ukiwa ni mchezo wa tano.


Mchezo wa kwanza walipokutana DR Congo,  ubao ulisoma AS Vita 0-1 Simba na bao lilipachikwa na Chris Mugalu kwa mkwaju wa penalti. 


Matola amesema:”Tunahitaji ushindi katika mchezo wetu wa kesho tunatambua ushindani utakuwa mkubwa ila tupo tayari.

Ameongeza kuwa wachezaji wote wapo fiti na hakuna ambaye watamkosa kwa sababu wale ambao walikuwa na majukumu katika timu zao za taifa wamerejea.


Miongoni mwa wachezaji waliokuwa na timu zao za taifa ni pamoja na Luis Miquissone raia wa Msumbiji, Clatous Chama raia wa Zambia, Meddie Kagere wa Rwanda, Mohamed Hussein, Shomari Kapombe, Aishi Manula walikuwa na timu ya Taifa ya Tanzania.


Kwenye kundi A Simba ina pointi 10 ikiwa nafasi ya kwanza na AS Vita ipo nafasi ya tatu na pointi 4 zote zinahitaji ushindi ili kufikia malengo ya kutinga robo fainali.

Simba inahitaji pointi moja kujihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali huku AS Vita wakihitaji pointi tatu kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali hivyo hautakuwa mchezo mwepesi.


SOMA NA HII  MIEZI SITA YA CHILUNDA NA SIMBA HII HAPA....ALIPEWA SHARTI LA KUPUNGUZA UZITO....