Home CAF ‘AS VITA TUPO TAYARI KUFUNGWA KESHO’

‘AS VITA TUPO TAYARI KUFUNGWA KESHO’


Benchi la ufundi la AS Vita limesema kuwa liko tayari kupokea matokeo yoyote kwenye mechi yao ya kesho dhidi ya Simba katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni

Kocha wa AS Vita, Florent Ibenge amesema kuwa hawako tayari kujiweka kwenye presha kubwa katika mchezo huo na aina yoyote ya matokeo yatakayopatikana watayapokea.

“Siku zote tumekuwa tukifurahia kucheza na ni furaha kubwa zaidi kucheza na timu kama Simba ambayo ni miongoni mwa timu bora na nzuri Afrika.

Tulicheza mechi ya kwanza kule DR Congo na tukashindwa kufanya kama tulivyotarajia tukapoteza mchezo hivyo tumekuja hapa tukiamini tukicheza kama tulivyopanga tutapata matokeo tunayoyahitaji.

Tunafahamu tunahitajika kupata ushindi ili tujiweke katika nafasi nzuri ya kufuzu lakini mwisho wa siku huu ni mpira wa miguu na tuko tayari kupokea matokeo yoyote iwe tutashinda, kutoka sare au kufungwa,” alisema Ibenge.

Kipa wa timu hiyo, Nathan Mabrouk alisema wanafahamu ugumu wa kucheza na Simba lakini wako tayari kukabiliana nao

“Wachezaji wote tuko tayari na akili yetu tumeilekeza kwenye mchezo huu ambao tunahitajika kupata ushindi,” alisema Mabrouk.

Vita yenye pointi nne, inahitaji matokeo ya ushindi tu katika mechi ya kesho dhidi ya Simba ili iweke hai matumaini yake ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu

SOMA NA HII  KISA KUZIMIKA ZIMIKA KWA TAA UWANJA WA MKAPA...CAF WATOA MSIMAMO HUU...