Home Burudani MANARA ATANGAZA KUONGEZA MKE WA TATU…”NINA NGUVU…NITAWAHUDUMIA”…

MANARA ATANGAZA KUONGEZA MKE WA TATU…”NINA NGUVU…NITAWAHUDUMIA”…


Baada ya kuongeza mke wa pili Alhamisi iliyopita msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara amefunguka mpango wa kuongeza mke wa tatu na wanne kwa sababu taratibu za dini zinamruhusu.

“Ikitokea nafasi nyingine kwa mujibu wa dini yangu na kama nitakuwa na uwezo wa kuwahudumia kibaiolojia na kifedha nitaongeza mke mwingine kwa sababu dini inaniruhusu,” amesema Haji Manara.

Hata hivyo safari hii, Manara hajatangaza kufanya sherehe kubwa kama ilivyokuwa kwenye harusi yake kwa mke wake wa kwanza, ambapo ilirushwa mbashara kwenye tv na mitandao ya kijamii.

Hii itakuwa ni ndoa ya nne kwa Manara , ambapo katika hizo ameshaacha na na wanawake wawili ambao pia alibahatika kupata nao watoto.

Katika ndoa zote hizo, hizi mbili za sasa na mbili zilizokufa, Manara amejaliwa kupata watoto watatu wanaotambulika.

SOMA NA HII  WAKATI NABI AKIWASILIZIA KAIZER CHIEF....MORRISON AIBUKA NA KUINGILIA DILI KWA NYUMA...