Home kimataifa MANCHESTER CITY INAMUHITAJI KANE, GREALISH

MANCHESTER CITY INAMUHITAJI KANE, GREALISH


IMERIPOTIWA kwamba kutokana na anguko la kifedha kwa timu nyingi England kutakuwa na mabadilishano ya wachezaji kwenye dirisha la usajili ili timu kutimiza malengo yao.


Hii imetokana na janga la Virusi vya Corona ambalo lilisababisha mechi nyingi kuchezwa bila mashabiki ili kuchukua tahadhari na hilo lilichangia kwa kiasi kikubwa uchumi kuyumba.

Miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa kuwa kwenye mabadilishano hayo ni pamoja na nyota ambaye anatikisa kwa sasa kwenye suala la usajili ambaye ni Harry Kane anayewindwa na Manchester City ambayo ipo tayari kufanya naye mabadilishano na Gabriel Jesus pamoja na Nathan Ake ili wapate saini ya mshambuliaji huyo.


Imeelezwa kuwa kuna makubaliano ambayo yanaweza kufikiwa kwa sasa na timu hizo mbili ambapo Kocha Mkuu wa City, Pep Guardiola anahitaji kuboresha kikosi chake na hesabu zake ni Kane na mshikaji wake Jack Grealish ambaye anacheza ndani ya Aston Villa.

Jesus mwenye miaka 24 hajawa na bahati chini ya Guardiola hivyo anaweza kuondoka kwenye kikosi hicho na Ake ambaye alisajiliwa kwa dau la pauni milioni 14 kutoka Bourrnemouth naye anaweza kuondoka

SOMA NA HII  RASMI....MBAPPE AFUNGUKA SAKATA LAKE NA NEYMAR...AKIRI KUNA MGOGORO KISA MESSI NA PSG....