Home kimataifa HATMA YA RAMOS REAL MADRD KUJULIKANA MWEZI HUU

HATMA YA RAMOS REAL MADRD KUJULIKANA MWEZI HUU


JUNI inaonekana kuwa itakuwa ni mwisho wa nyota wa kikosi cha Real Madrid, Sergio Ramos kufahamu kwamba atabaki ndani ya kikosi hicho ama atasepa mazima.

Mkataba wa nahodha huyo ndani ya kikosi hicho unameguka mwezi huu na mpaka sasa hakuna dalili zozote za kuzungumzia mkataba huo.

Ramos mwenyewe wala Madrid hakuna ambaye ametoa taarifa kuhusu ishu ya dili lake hivyo mwezi huu hatma yake itajulikana namna itakavyokuwa.

Ramos alijiunga na timu hiyo 2005 na amekaa kwa zaidi ya miaka 15 na amefanikiwa kutwaa mataji 22 pia ana mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

SOMA NA HII  NAHODHA WA ASTON VILLA AREJEA KIKOSINI