Home Uncategorized CHIRWA AIFANYIA MAAMUZI MENGINE YANGA

CHIRWA AIFANYIA MAAMUZI MENGINE YANGA


MAMBO yamemnyokea mshambuliaji wa Azam FC Obrey Chirwa baada ya kuelewana na kukubaliana kusaini mkataba wake mpya na klabu hiyo tukio ambalo litafanyika Jumamosi.

Awali Chirwa ambaye ni Mzambia ligoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo na inatajwa kuwa malengo yake yalikuwa ni kutaka kurejea Yanga lakini kocha Zahera akamkaushia.

Chirwa aliwahi kuichezea Yanga kabla ya kutimkia Misri kisha kurejea na kujiunga na Azam FC msimu huu katika ligi amefunga jumla ya mabao matatu.

Mratibu wa Azam FC, Philipo Alando alisema kuwa tayari wameongea na wachezaji kinachosubiri wa sasa ni kusaini tu na kuendelea na mambo mengine.

“Unajua kila kitu kina kwenda sawa Chirwa pamoja na wenzake tumeshaongea nao na kutakubaliana kilichokuwa kinasu biriwa ni wao kuweza kusaini mikataba yao na kundelea na mambo mengi,”alisema Alando ambaye ni mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar na Azam.

Uwepo wa taarifa hizi unaleta ugumu wa Chirwa kurejea katika klabu yake ya zamani ambayo ni Yanga baada ya kuwepo kwa tetesi zilizoelezwa kuwa angesajiliwa na mabingwa wa kihistoria kunako ligi kuu.

SOMA NA HII  BERNARD MORRISON AFUNGUKIA USAJILI WAKE SIMBA