Home Simba SC MKUDE YUPOYUPO SANA SIMBA, MKATABA WAKE BADO UNAISHI

MKUDE YUPOYUPO SANA SIMBA, MKATABA WAKE BADO UNAISHI

SULEIMAN Kova, Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Simba amesema kuwa wanaosema kwamba kamati inamkomoa kiungo mkabaji Jonas Mkude  hiyo sio sawa na suala la mkataba wake kukaribia kuisha bado sana.

Mkude amesimamishwa ndani ya Simba kutokana na tatizo waliloeleza kuwa ni utovu wa nidhamu na anatakiwa kwenda Muhimbili kufanyiwa vipimo ili kujua tatizo linalomsumbua kwa kuwa amekuwa akifanya makosa mara kwa mara.

Kova amesema:”Kuna watu nimeskia katika maoni yao wanafikiria labda mkataba wa Mkude unakaribia kuisha kwa hiyo Simba au sisi tunatumika kumkomoa mchezaji.

“Nimeangalia mkataba wa Mkude bado ni mbichi kabisa, ni mchezaji anayependwa na kila Mwanasimba lakini linapotokea tatizo ni lazima lishughukikiwe,”.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa nyota huyo ambaye hivi karibuni aliongezewa mkataba wake na Simba ambao bado unampa uhai wa kuendelea kuitumikia Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, raia wa Ufaransa.


SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIKODI NDEGE KWENA NIGERIA...SIMBA WAINGIA MKATABA WA MAMILIONI NA AIR TANZANIA