Home Simba SC WACHEZAJI SIMBA WAPUNGUA MOROCCO

WACHEZAJI SIMBA WAPUNGUA MOROCCO


PATRICK Rweyemamu, meneja wa Simba amesema kuwa wanaendelea vema na kambi nchini Morocco huku changamoto kubwa ikiwa ni kupungua kwa wachezaji. 

Kupungua kwa idadi ya wachezaji hao inatokana na kuitwa kwao katika timu zao za taifa kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia.

Kwa Tanzania wachezaji walioitwa wanatakiwa kuripoti kambini mapema Agosti 24 kuanza maandalizi hayo chini ya Kim Poulsen ambaye ni Kocha Mkuu wa Tanzania.

Miongoni mwa nyota wa Simba ambao wameitwa katika timu ya taifa ya Tanzania ni Israel Mwenda, Aishi Manula, Mohamed Hussein,  Shomari Kapombe na John Bocco.

Rweyemamu amesema:”Maandalizi ya kambi yanakwenda vizuri na kila kitu kipo sawa hasa kwa wachezaji kufuata kile ambacho wanaambiwa na kuendelea zaidi na mazoezi. 

“Changamoto kubwa kwa sasa ni kupungua kwa kikosi kwani kuna wachezaji ambao wanakwenda kuripoti katika timu zao za taifa.  Tunajua kwamba Simba ina wachezaji ambao wameitwa katika timu zao za taifa ikiwa ni pamoja na Uganda, Kenya hivyo hiyo changamoto tunakwenda nayo sawa ili tujue inakuaje.

“Mechi yetu dhidi ya FAR Rabat ilikuwa ni kwa ajili ya ufundi zaidi kwa kuwa wachezaji walikuwa wanatazamwa kile ambacho wamepewa na haikuwa mbele ya mashabiki zaidi ilikuwa ni mechi ya ndani,” .

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIWA NA HOFU KUHUSU SAFARI YA AFRIKA KUSINI..SERIKALI WAIBUKA NA TAMKO HILI...