Home Uncategorized SPURS YAGOMEA KUSHUKA CHINI, KUVAANA NA VINARA

SPURS YAGOMEA KUSHUKA CHINI, KUVAANA NA VINARA

 


JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Tottenham sasa ameanza kutamba baada ya timu yake kuonekana inaweza kushindania ubingwa msimu huu, katika Premier League.

 

Bosi huyo wa Spurs aliiongoza timu yake mbele ya mashabiki 2,000 kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal, usiku wa Desemba 6 na kuifanya iwe nafasi ya kwanza na pointi 24 baada ya kucheza mechi 11.

Kesho Spurs itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Antwerp ila ni mchezo wa Europa League ambapo ikiwa nafasi ya pili na pointi 10 inakutana na vinara wa kundi J wakiwa na pointi 12.


Mourinho amesema: “Watu wengi wanaweza kufikiria mechi tatu ngumu tulizocheza mfululizo dhidi ya Manchester City, Chelsea na Arsenal kwamba ulikuwa ni wakati wetu wa kupoteza pointi na kurejea kwenye nafasi ya kuwa timu ya kawaida.

 

“Lakini hatujarejea kule walikokuwa wakifikiria, tuko hapa na tutaendelea kuwa hapa.”

 

“Wachezaji wangu wanafanya kazi kama wanyama, nawaheshimu wanyama, msije mkanifikiria vibaya, wanafanya kazi nzuri hata kama wakiwa hawana mpira,” .

SOMA NA HII  KIKOSI CHA JKT TANZANIA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA SIMBA